HALI TATU ZA MAADA
Maada
Ni kitu chochote chenye uzito na
kinachoshika nafasi.mf jiwe,kalamu,maji,mafuta nk.
Aina/namna/Hali
za maada
1.
Yabisi
2.
Kimiminika
3.
Gesi
Yabisi
ni hali ya maada
ambayo ina msongamano mkubwa wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada.mf.jiwe,barafu,kiti,karatasi
nk.
Sifa za maada yabisi
·
Ina msongamano
mkubwa wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada (atomi)
·
Ina umbo maalumu
·
Ina ujazo maalumu
·
Molekyuli haziko huru kutembea ila kutetemeka tu
·
Haiwezi
kugandamizwa
Maada kimiminika
Ni
hali ya maada yenye msongamano wa wastani wa chembe chembe ndogo ndogo sana
zinazounda maada (atomi/molekyuli).mf. maji,mafuta ya taa,mafuta ya
petrol,maziwa ya wanyama.nk.
Sifa za maada kimiminika
·
Ina msongamano wa
wastani wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada
·
haina umbo
maalumu,umbo lake hutegemea umbo la chombo kilichobeba maada
·
Ina ujazo maalumu
·
Molekyuli ziko
huru wastani katika kutembea
·
Molekyuli
zinaweza kugandamizwa kidogo sana
Maada ya gesi
Ni hali ya maada ambayo ina msongamano
mdogo sana wa atomi/molekyuli.mfano gesi zote kama
kabonidaioksaidi,oksijeni,haidrojeni,mvuke nk.
Sifa za maada gesi
·
Ina msongamano
mdogo wa molekyuli/atomi
·
haina umbo
maalumu
·
haina ujazo
maalumu
·
Molekyuli ziko
huru kutembea
·
Molekyuli zinaweza kugandamizwa kwa kiasi kikubwa
Aina za mabadiliko katika maada
1.
Badiliko
la kiumbo
2.
Badiliko
la kikemikali
Badiliko la kiumbo: ni aina ya badiliko katika maada
ambalo si la kudumu.mf kuungua kwa mshumaa,kuyeyuka kwa barafu.
Badiliko la kikemikali:ni aina ya badiliko katika maada
ambalo ni la kudumu.mf.kuungua kwa karatasi,chuma kupata kutu,kuchacha kwa
maziwa ,nk
Tafauti
kati ya badiliko la kiumbo na la kudumu
Badiliko la kiumbo
|
Badiliko la kikemikali
|
I.
sio la kudumu
II.
Uzito wa kitu haubadiliki
III.
Kitu kipya hakitokei
IV. Tabia ya kitu haibadiliki
baada ya badiliko
|
I.
Ni badiliko la kudumu
II.
Uzito wa kitu hubadilika
III.
Kitu kipya hutokea
IV. Tabia ya kitu hubadilika
baada ya badiliko
|
Asante
ReplyDeleteAppreciate it
ReplyDeleteNaomba matumizi ya badiliko la kiumbo na kikemikali
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteNimependa
DeleteNaomba sababu zinazopelekea maada kubadilika kutoka hali moja na kwenda nyengine
ReplyDeleteNaomba tofauti kati ya yabisi na ges na kati ya hizo ipi huwa ni nyepes
ReplyDeleteHakuna nyepesi endapo uzito huwa sawa ila ujazo ndo huwa tofauti
DeleteAsante sana
ReplyDeleteNaomba mchoro unaoonesha hali hizi tatu za maada na mifano yake
ReplyDeleteAsante Kwanzaa Kwa kunielimisha
ReplyDeletenaomba zana za kufundishia na kujifunzia hii mada MAADA
ReplyDelete