Posts

Showing posts from October, 2017

HALI TATU ZA MAADA

Image
Maada Ni kitu chochote chenye uzito na kinachoshika nafasi.mf jiwe,kalamu,maji,mafuta nk. Aina/namna/Hali za maada 1.       Yabisi 2.       Kimiminika 3.       Gesi Yabisi ni hali ya maada ambayo ina msongamano mkubwa wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada.mf.jiwe,barafu,kiti,karatasi nk. Sifa za maada yabisi ·          Ina msongamano mkubwa wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada (atomi) ·          Ina umbo maalumu ·          Ina ujazo maalumu ·          Molekyuli  haziko huru kutembea ila kutetemeka tu ·          Haiwezi kugandamizwa Maada kimiminika Ni hali ya maada yenye msongamano wa wastani wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada (atomi/molekyuli).mf. maji,mafuta ya taa,mafuta ya petrol,maziwa ya wanyama.nk. Sifa za maada kimiminika ·          Ina msongamano wa wastani wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada ·          haina umbo maalumu,umbo lake hutegemea umbo la chombo kilichobeba maada ·